HITAJI LANGU,SEHEMU YA 001

10/05/2016 11:58:00 pm
HITAJI LANGU
Na: Fraidy Mtemah
Tel: 0716883222
SEHEMU YA 001.
“whaaat……!!!, Zuuu……!!?” ni mshangao alioupata John ghafla baada ya kufungua mlango wake Wa chumbani akitokea bafuni huku taulo likiwa kiunoni na kumuona dada yake Zulpha amekaa kitandani kwake. Kutokana na heshima ya wawili wale ambayo ilithibitishwa kwa kuitana dada na kaka pia muda maana ilikuwa majira ya saa tano na dakika zake ya usiku, john aliona wazi amevunjiwa heshima hali iliyompelekea kuchukia ghafla bila kujua kuwa dada yake alikuwa na tatizo gani hadi akawa chumbani kwake na siyo mazoea yake.

“samahani dada yangu naomba utoke ndani ya chumba changu”
alizungumza kwa sauti ya upole ila ilikuwa imetawaliwa na hisia za hasira. Hata hivyo Zulpha aliyekuwa anapenda sana kuitwa Zuu alikuwa bado amekaa kwenye kitanda cha kaka yake huku macho yake akiwa ameyaelekeza kwenye kioo kilichopo ukutani usawa wa mbele yake. Hazikupita dakika tatu macho ya Zuu yalianza kutiririsha machozi, ambapo sauti za kuvuta kamasi zilianza pia kuyasindikiza machozi yale. Kilio cha ndani kwa ndani kilidhihilishwa kwa kwikwi.
John alimtazama kwa muda, ghafla hasira zake ziliyeyuka mithili ya njozi ya mchana aotayo mtu na kushituka kwa kuitwa kuwa chakula tayari.aliwaza ila hakuwa na jibu, hatua kadhaa alizipiga toka mlangoni aliposimama hadi jirani na dada yake Zuu. Aliweka pembeni nguo yake ya ndani (boxer) aliyokuwa ameishika akitoka nayo bafuni kisha alipiga magoti na kuanza kumfuta machozi dada yake Zuu kwakutumia viganja vya mikono yake. Kitendo kile kilimfanya Zuu aongeze spidi ya kulia. John alimbembeleza na kumnyamazisha kisha alimwambia
“tukio unalolifanya sasa ni mfano wa kitendawili ambacho jibu unalo wewe.mimi ni kaka yako, tumetoka mbali sana naomba nieleze tatizo nini hadi usiku huu upo hapa?” aliishia kumuuliza shwali kisha kusubiri jibu huku akiendelea kumchezea viganja vya mikono yake kwa lengo la kumfariji na kumshawishi aweze kuzungumza tatizo alilonalo. Kweli Zuu alizungumza
“kwanza samahani kwa kuingia chumbani kwako bila ruhusa, najua kama nimekukosea nisamehe sana”
“bila samahani”
“nimekuja kukuaga kesho nasafiri” alizungumza na kuinamisha kichwa chini
“unasafiri….!!!? Mbona ghafla, halafu tumeshinda wote kutwa ila taarifa unanipa usiku namna hii? Ok…! Unaenda wapi na wazazi wanafahamu?” bado John alikuwa katika hali ya sitofahamu kwa kilichokuwa kikiendelea
“swala la kufahamu wazazi wala halina umuhimu kama wewe, pia kusafiri kwangu ghafla ni kutoka na sababu kunijia ghafla” alimaliza kwa kuvuta kamasi na kushusha pumzi kwa taratibu
“wazazi hawana umuhimu? Je unaelekea wapi , kufanya nini na utarejea baada ya muda gani?”
“sijui nitaelekea wapi, sijui ninaenda kufanya nini na wala sijui nitarejea lini. Lakini ukweli ni kwamba, sababu inayonifanya nisafiri ni wewe kushindwa kutambua hisia zangu za kimapenzi. Kwanini hunipendi? Ninakasorogani? Ni bora ningekuona hata na mwanamke ningesema unaupendo wa kweli kwa mpenzi wako lakini tumekuwa wote wala sijashuhudia kitu kama hicho.” Ni maelezo yaliyomchanganya kichwa John kwa haraka aliwaza mbali sana kisha alichoka.
“kwahiyo swala la wewe kunipenda namimi kutokukubalia ndilo linalokutoa nyumbani?”
“ni hilo tu wala hakuna lingine.naaa…., nikutakie usiku mwema ila nisikuweke katika matatizo kuwa endapo wazazi wakikuuliza niko wapi wambie hufahamu,ukijipendekeza kuzungumza chochote utateseka sana sipendi iwe hivyo. Ahsante” Zuu alimaliza kuzungumza kisha alisimama na kuondoka kwa haraka. John alijitahidi kuinuka kwa haraka na kumshika kabla hajafungua mlango. Pulukushani za hapa na pale ili atulie kisha azungumze naye jambo lolote, mala taulo lake lilifunguka na kuanguka kisha Zuu alimgeukia na wakawa wanatazamana uso kwa uso hali iliyomfanya John awe mzito kuinama na kuokota taulo kisha kuishia kutazamana.
Zuu hakujizuia, alimtazama John taratibu kuanzia pale usoni hadi kwenye vidole vya miguu kisha kumpandisha tena na kumuona mwili wake barabara.macho yale ya Zuu baada ya kufaidi vingi, yaliishia tena machoni kwake mara yalishuhudia macho ya John yakitiririsha machozi. Alitoa chozi kwa uchungu kutokana na kitendo kile hakutarajia kama siku moja atakuja kudharirika kiasi kile. Ingawa walikuwa wawili tu ila walikuwa ni mtu na dada yake ndiyo maana aliumia sana moyoni mwake. Akiwa bado mtupu alimwambia
“ahsante sana” kisha aliinama, aliokota taulo na kujifunga. Aligeuka na kurejea kitandani kwake. Alipojitupa na kutazama tena mlangoni hakumuona Zuu alikuwa amekwisha toka.
Usiku ule John alikuwa katika hali ya mawazo sana aliwaza kile alichokuwa akikitaka Zuu kuwa wawe wapenzi aliona haiwezekani, aliwaza endapo akiondoka wazazi watakuwa katika hali gani maana walikuwa wanampenda sana binti yao, aliwaza pia yeye atakuwa katika mazingira gani endapo Zuu hatakuwepo nyumbani, mwisho wa yote alipta jibu kuwa amani itapotea kuanzia nyumbani hata katika maisha yake kwa ujumla. Jibu lile lilimfanya akeshe macho kumchunguza Zuu kama kweli ataondoka usiku.
saa sita na nusu ya usiku John alihisi mtu anatembea kwenye korido, alipochungulia alimuona Zuu ndiyo anafunga mlango wa nje na kuanza safari. Alirudi na kuvaa haraka kisha kuanza kumfatiria. Zuu alinyoonsa barabara ndogo ambayo mchana huwa na msongamano sana wa watu ila usiku huwa tulivu ambayo kuanzia relini hutokezea kwa azizi ally stand. Uzuri wake ni kwamba kuna bajaji zilizokuwa zikikesha usiku kucha. Alipofika kwenye lound about ya kwaazizi Azzy alichukua bajaji moja na kuanza safari. John alipoona vile alimuacha umbali flani kisha naye alichukua bajaji na kumwambia waifukuzie bajaji iliyotangulia lakini wasiikute wala kuipita.
Bajaji ziliendeshwa na kutokezea Mandela road walishika njia hadi tazara kisha kuitafuta buguruni. Ziliendelea kushika njia hiyo zikielekea Ubungo stand ya mkoa.
“niache hapa hapa” John alisikika akimwambia dereva bajaji mara baada ya kufika kwenye mataa ya Ubungo. Alishuka na kuelekea stand ya mkoa ambako alimuona Zuu ameelekea huko. Alipofika getini alitakiwa alipie sh.200 ili aingie ndani ila kwa bahati mbaya alipotazama pesa mfukoni hakuziona kumbe alipomlipa Yule dereva bajaji na kuzirejesha pesa mfukoni bahati mbaya hazikuingia vizuri hivyo alivyokuwa akikimbia zilianguka.
Aliwaomba walinzi ili wamruhusu apite ila hawakumuelewa, alibaki ameduaa. Akiwa katika hali ya mawazo muda ulizidi kuyoyoma ambapo magari yalianza kujipanga foleni kuruhusiwa kutoka na kuanza safari za mikoani. Hiyo inatokana na utaratibu maarumu waliouweka pale stand ya mkoa ili kuzuia magari kusafiri usiku sana kwa lengo la kuimarisha usalama. aliwaza tena mbona watanzania watu wema sana, atashindwaje kupita pale kwa kikwazo cha sh.200 tu? Alimfata mmoja wa msafiri aliyekuwa akiingia alimuomba amsaidie kweli alimlipia kisha kuruhusiwa kuingia. Akiwa ndani ya stand John alianza kuingia kwenye kila basi Na kumuangalia. Baada ya kutazama magari mengi bira mafanikio, kwa bahati nzuri gari la Saba alibahatika kumuomba.
" samahani sana Zuu, kwa heshima yangu nakuomba tushuke unisikilize kisha uendelee Na safari yako. Sitotaraji kumpata jibu la hapana kwasababu hukutaraji kama muda huu ningekwepo hapa hivyo ni Jambo leyeuzito mkubwa sana". Kweli Zuu hakuamini machoyake Mara baada ya kumuona John ndani ya lile gari pia kuyasikia maneno Yale aliyoyazungumza. Alimtazama kisha alimwambia
"Kwanini anashindwa kunielewa?, kwanini unanifanya mtoto mdogo? Nimeanza kukueleza hisia zangu tangu mwaka gani? Nimevumilia sana John sasa ifike mwisho naomba niache niendelee Na safari yangu huna jipya utakaloweza kunieleza hadi nikakuelewa endapo nitashuka." Alimaliza kuzungumza kisha alichukua ear phone za Simu yake na kuziweka vyema masikioni mwake.
Kwa Mara nyingine tena John aliona amedharaulika ila hakupiga moyo konde alimtoa zile ear phone kwenye masikio kisha kumbembeleza sana. Wakiwa bado kwenye majadiliano hayo ya kubembelezana Mara magari yaliruhusiwa kuanza safari hali iliopelekea gari lile aina ya Super Feo iliyokuwa ikielekea mbeya kutoka stand na kushika njia kuu ya mikoani huku John naye akiwa ndani. Kabla halijavuka taa za pale Ubungo Zuu alikubari kushuka baada ya kunong'onezwa Jambo zuri.
"Haya nieleze hilo lamuhimu kwako" alizungumza kwa dharau Sana. John alivuta pumzi Na kuishusha kisha alizungumza kwa upole sana
"Hakuna chenye mwanzo kikakosa kuwa Na mwisho. Thamani ya jua huonekana pindi wingu liyeyukapo, vilevile harufu nzuri ya chakula haina thamani kwa aliyeshiba."
"Mbona sikuelewi acha kunipotezea muda bwana" alizungumza kwa jazba.
"Pole sana kwamaana hapo ndipo upeo wako ulipoishia.umenizoea sana Dada yangu Na haya ndiyo matunda yake. Lakini usijali ukweli ni kwamba, zulpha kwa uelewa wako anafahamu wazi uhalisia wa maisha yangu, ila ukweli ni kwamba ingawa tumeishi kwa kukuwa wote ila bado hufahamu kwa undani maisha yangu. Machache uliyoyafahamu kuhusu mimi ni kutokana na chuki za mama kwangu imepelekea wewe kujua mapema maisha yangu hadi kupelekea unidharau namna hii. Sina nia yakwamba mama aonekane mbaya kwako au kwa Baba, lakini Leo nimelazimika kukueleza ukweli kwasababu bila mama kukueleza lolote kuhusu mimi wala usingenipenda kimapenzi pia tungeendelea kuheshimiana kama kaka na Dada. Mbona mwanzo tulikuwa tunaheshimiana vizuri? Watu walikuwa wanatuita mapacha, iko wapi furaha Ile ya mwanzo kwenye maisha yetu, kwa Azizi Ally nzima wanajua Mimi na wewe ni mtu na Dada yake sasa Leo ikaonekana wapenzi jamii itatuchukuliaje? Zuu Dada yangu hebu rudisha moyo wako nyuma nipethamani ya kaka moyoni mwako chukua damu zetu zifanye ni muunganiko wa chembechembe hai zisizoweza kutengana. Nahitaji faraja moyoni mwangu Zuu,nahitaji kuwa nawe Dada yangu, kuishi mbali nawe ni kama pigo kwangu. Tafadhali naomba nielewe"
Wakati anazungumza hayo yote Zuu akuwa ameipakata mikono yake tumboni, macho ameyainua juu huku akizungusha kichwa kulia na kushoto kanakwamba hasikii wala haelewi chochote kilichokuwa kikiendelea.hata hivyo John aliendelea kujimaliza
"Hebu fikiria kwa baba na mama mpo watoto wangapi? Je ninani atakayekuja kukutembelea kamandugu yako pindi utakapoolewa? Furaha ya Ndugu haifananishwi NA furaha ya rafiki wala jirani. Amini mimi ni nduguyo nahitaji Dada yangu uolewe na nije kukutembelea nawe ujivunie una kaka. Usitengeneze mazingira ya upweke kwenye Ndoa yako. Nakupenda sana Dada yangu naomba turudi nyumbani, ukarejeshe furaha ya nyumba naamini wazazi hawatakuwa na maelewano endapo wakigundua haupo."
Baada ya maelezo ya muda mrefu sana ndipo Zuu alipoweza kushawishika, akarudisha moyo Na kukubaliana Na matokeo. Aliamua kurejea nyumbani. Wakiwa kwenye daladala John alikuwa Na furaha sana moyoni mwake kwani hakutegemea kama mwisho wa Yale yote ni Zuu kukubaria kuahirisha safari yake.
Majira ya saa mbili kasoro ya asubuhi walifika nyumbani ambapo waliwakuta wazazi wao wakijadiliana kuhusu wao. Walipoingia tu mama alikuwa wa kwanza kuonyesha kuwa amekasirika Hali iliyompelekea kuwapokea kwa swali.
" mmetoka wapi? Na wewe Malaya umetoka wapi Na binti yangu?" Lamwisho Lilikuwa swali lililomkasirisha kila mmoja aliyekwepo pale.
" mke wangu ni maswali gani hayo? Hivi unajua kama hawa ingawa ni watoto wetu ila ni watu wazima? Kuwa mpole tukae nao chini tuzungumze nao tutapata jibu lakini siyo kwa style hiyo. Sijapenda kabisa tena usirudie tena kutoa kauli chafu namna hiyo. Vijana karibuni mkae" alizungumza Baba yao ambapo Zuu alijivuta hadi kwenye sofa Na kukaa ila John uvumilivu ulimshinda, akiwa bado amesimama akijikuta tu machozi yanamtoka. Wakiwa bado wanatazamana huku mioyoni mwao wakielekeza chuki kwa mama, Mara John akiwa bado anateremsha chozi alizungumza
"Nilizaliwa na mama,Mara nyingi niwapo usingizini huzungumza na Mama.hunisihi mengi sana na hayo ndiyoyanayonifanya nizidikukuheshimu wewe Mama yangu kika kukicha, kamwe sitokuja kukuvunjia heshima wewe ni Mama yangu na huyu ni Baba yangu. Nawaombeni mnipe dakika tano nitarejea." Alipomaliza kuongea hayo alinyoosha chumbani kwake huku akiwaacha katika Hali ya sitofahamu.
Wakati John yupo ndani huku nyuma Baba alimuuliza mwanaye
"Zulpha binti yetu kipenzi mmetoka wapi asubuhi yote hii huku ukiwa na begi wakati Jana tuliagana wote tunaingia kulalama?"
"Ni story ndefu Baba na Mama yangu ambayo kunajambo imedumu kwa muda Wa miaka 10 Na sasa lilikuwa inaanza kutimia." Jibu lile liliwashangaza wazazi wake wote wawili
" miaka 10!!? Unamaana gani Na ni Jambo lipi hilo!?" Alihoji tena Baba
"Utalijua Baba kwanza nianze kuwafahamisha kuwa bila jitihada za John hadi muda huu msingefahamu wapi nilipo pia sizani kama mngenipata kwa urahisi. Nasemahivi kwasababu maisha yangu nilisha..............!" Alikatisha maongezi baada ya kumuona John anatoka na begi analivuta huku dogo likiwa mgongoni.kitendo kile kilimfanya kila mmoja apigwe na bumbuwazi. Baba alisimama na kumgeukia.
"Unawazimu.......!!!! Au......!!!?" Ni swali alilotoa Mzee ambalo halikutarajiwa hata siku moja. John aliendelea kujongea hadi karibuni yao. Alipofika aliweka mabegi yake pembeni kisha alimwoma Baba yake akae, alifanya hivyo kisha naye alipiga magoti Mbele yao akawambia.
"Wazazi wangu ninanafasikubwa ya kuwashukuru kwamaana sina wazazi wengine zaidi yenu. Ninanafasi kubwa yakuwaita nyinyi ni wazazi wangu wakunizaa kwamaana tangu nilipoanza kutazama nilianza kuwaona nyinyi, hadi sasa ninamiaka 27 bado nawaona nyinyi, hivyo naamini nyinyi ni wazazi wangu wa kunizaa.sababu nyingine yakuwaamini wazazi wangu nikwamba nyinyi ndiye mnayejua historia yote ya maisha yangu. Baba unaijua vizuri pia Mama unaijua vizuri. Mmenilea vizuri hadi Leo hii najitambua.sina chakusema niwalipe maana hata ningesema ninauwezo wakuwapa dunia muimiliki wala isingeweza kutosha kuwa zawadi ya vile mlivyonilea. Ila nathubutu kusema Mungu awalipe,hiyo naamini ni zawadi ya pekee ambayo inaweza kuchukua nafasi kubwa.
Lakini kabla sijawaweka wazi kile nilichokusudia kukifanya naomba niwaweke wazi kuwa saizi mmeniweka katika wakati mgumu. si Baba Mama wala Dada yangu Zuu nyote mmeniweka katika wakati mgumu.sina furaha tena na siwezi kuchukua maamuzi juu ya lolote mpendalo nyinyi ndiyo maana nimechukua maamuzi haya myaonayo hapa.nashukuru kwakuweza kuishi nanyi kwa amani na upendo hivyo nimeamua kwenda kujitegemea."
Mazungumzo Yale bado yaliwaacha njia panda,wazazi hawakujua kwanini John amefikia uamuzi ule ila Zuu alikuwa akifafahamu. Ingawa Zuu alikuwa akifahamu ila yeye ndiye alikuwa anaumizwa sana na uamuzi ule Wa John. Baba alimwambia
" Mimi ndiyo Baba yako na huyu ndiyo Mama yako mwenyewe umelithibitisha hilo sasa hauwezi ukachukua maamuzi yako bila idhini yetu. Kama kuna tatizo nilazima uliweke wazi kwetu kisha tulitatue. Siyo unachukua maamuzi mkononi kisa umekua je ungekuwa na miaka mitano ungefanya hicho unachotaka kukifanya? Haya tueleze tatizo nini."
John alikuwa katika wakati mgumu kueleza kile kilichomsibu lakini kutokana na kauli za wazazi wote wawili hakuwa na jinsi alilazimika kuongea ingawa ilikuwa na athari kubwa kwake na kwenye familia Ile kwa ujumla.
"Ukweli Ni kwamba Zuu ananimenda kimapenzi, ingawa siyo Jambo lakushangaza ila imefikia kipindi nisipomkubalia yupo tayari kuchukua maamuzi magumu dhidi ya maisha yake. Hali hii inanitatiza kwakuwa binafsi namheshimu kama Dada yangu pia jamii inatuchukulia hivyo kuwa sisi ni Ndugu. Jambo hili limenza mda mrefu sana nilijitahidi kulitatua kadri ya uwezo wangu ila limenishinda.
Nikija kwa Mama niwazi umeniwekea chuki mwanao. Naamini chukihiyo imepeta nguvu Mara baada ya kuhisi Zuu anataka kuwa na mahusiano ya kimapenzi nami. Najua umemueleza mengi Zuu juu yangu hadi ilifika kipindi alianza kunidharau. Hiyo pia nisababu inayoniweka katika wakati mgumu na kushindwa kumuelewa Zuu hitaji lake. Haiwezekani nikawa ninauhusuano na Zuu huku Mama akiwa hapendi. Amani haitakwepo humu ndani.
Kwako Baba wewe ndiyo inanitatiza zaidi kwasababu wewe unajua kwakina thamani yangu na undani Wa maisha yangu Hali inayokupelekea kunipenda sana. Sasa wakati wewe unanipenda halafu ni kichwa cha nyumba hapohapo Mama na Dada wanakinyongo na Mimi unawatengenezea mazingira ya kunichukia Mara mbili. Nashukuru sana Baba yangu kwa upendo anaouonyesha kwangu ila upendo huohuo ndio unaonitesa zaidi kupitia hawa wawili.
Hivyo basi nimeamua niondoke ila vitakuwa nakuja kuwasalimu. Naombeni mnisamehe pale nilipokosea pia naomba niwaache na amani ndani ya nyumba Mimi sasa naondoka naenda kutafuta maisha Mbele ya safari.samahani kama nimewakwaza pia Ahsanteni kwa kunisikiliza.
Wote walibaki hoi Mama na mwanaye Zuu walikuwa wameinamisha vichwa chini. Baba alilifikiria kwa kina kisha alimwambia
"Mwanangu hilo tumelisikia ila kwakuwa Mimi ni Baba Wa hii familia nakuomba rudisha mizigo ndani kisha nitalifanyia kazi hilo. Kama anahitaji kuondoka utaondoka ila tukiwa tumeridhika na sisi wazazi wako.
" sawa Baba ila naomba lichukulie uzito hilo" alisisitiza John
" nimekuelewa ndani ya siku mbili hizi utapata jibu na yatakuwa yameisha kabisa"
Walimaliza mazungumzo na Baba aliekekea kazini.
**********************
je! John ni mtoto wa familia Ile?
Je niyepi maamuzi atakayoyachukua Baba akiwa kama kichwa cha familia?
Hayo na mengine mengi......
USIKOSE SEHEMU YA 002

Kwa ushauri ushauri na maoni no. 0716883222

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng