Na: Fraidy Mtemah
Tel: 0716883222
SEHEMU YA 002.
Ilipoishia>>>>>>>>>
"Mwanangu hilo tumelisikia ila kwakuwa Mimi ni Baba Wa hii familia nakuomba rudisha mizigo ndani kisha nitalifanyia kazi hilo. Kama anahitaji kuondoka utaondoka ila tukiwa tumeridhika na sisi wazazi wako.
" sawa Baba ila naomba lichukulie uzito hilo" alisisitiza John
" nimekuelewa ndani ya siku mbili hizi utapata jibu na yatakuwa yameisha kabisa"
Walimaliza mazungumzo na Baba aliekekea kazini.
Inaendelea >>>>>>>>>
Akiwa kazini Baba Zuu aliyekuwa anaitwa Shaban akili yake haikutulia. Kila alipojitahidi kufanya kazi wala hakuweza. Akili yake ilikuwa imeshavurugika kutokana na matatizo ya familia ambayo yalikuwa yanamtegemea yeye kuwa mtatuaji mkuu. Aliwaza juu ya John ambaye kulikuwa na siri kubwa aliyekuwa anaifahamu yeye mwenyewe. Alikuwa katika wakati mgumu kuchukua maamuzi juu ya John kuondoka pale nyumbani. Lilikuwa shwala ambalo haliwezekani kutokana na siri aliyonayo ila kwa upande wa pili aliona wazi John lazima ataondoka pale.
Mr.Shaban alizidi kuumia kichwa juu ya mkewe mpendwa aliyetokea kumpenda bila mfano. Hakupenda awe anachukua uamuzi wa Jambo lolote pasi kushirikiana na mkewe. Lakini hili la John lilikuwa gumu kumshirikisha mkewe hata kwakujadiliana tu. Kuna siri ambayo hakupaswa ajue ambayo ilibeba mambo mengi juu ya muunganiko Wa maisha ya John na familia yao. Aliwaza endapo mkewe angeifahamu siri hiyo basi angefurahi sana kwa maana ameshagundua kuwa anamchukia John hivyo angechukulia kama kigezo cha kumfukuzia John katika Ile nyumba.
Vilevile alielekeza fikra zake juu ya bintiye wapekee ambaye yeye na mkewe walitokea kupenda mno. Binti Yule walimpata kwashida sana, siyo kwamba walikuwa hawana uwezo Wa kumpata mtoto ila kabla ya Mama Zuu kumzaa Zuu alipatwa na ugonjwa ambao ulishambilia mfumo wake Wa uzazi, hali iliyompelekea kukaa miaka mingi bila kushika ujauzito. Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu alifanikiwa kushika ujauzito ambao ilikuwa chini ya uangalizi maalumu tangu alipoupata hadi alipojifungua mtoto ambaye ni Zulpha. Jitihada kubwa za madaktati huku yeye na mumewe wakiwa makini katika kuhakikisha wanafuata maagizo ya daktari ndizo zilizopelekea ujauzito ule kukuwa vyema pasi na misukosuko yoyote hadi kujifungua salama salimini.
Furaha ya pekee ilitawala kwenye nyumba na familia Ile kwa ujumla juu ya kumpata mtoto Zulpha. Utata ulikuja wakati wa kumtafutia jina mtoto, Mama alitaka litoke kwake Baba nae alitaka litoke kwake. Utata ule ulipelekea majina toka pande zote mbili yawekwe mezani kisha wapige Kura jina lipi zuri. Kwa bahati nzuri walilipata jina moja ambalo Mama alionekana kunipenda zaidi kuliko Baba hata hivyo Baba alikuwa mpole kwa lengo la kumridhisha mkewe. Kweli jina walimuita mtoto ila kwabahati mbaya mtoto alikuwa akilia sana kila walipomuita jina hilo. iliwalazimu wazee waanze kumuita majina yote yaliyopendekezwa yani moja baada ya lingine, hatimaye waliangukia kwenye jina la Zulpha ambalo lilipendekezwa toka upande wa Baba. Mama hakuwa na nyongeza alichokifanya ni kukunjua moyo akakubali mtoto aitwe jina lile.
Zuu alipofika umri wa miezi sita Mama alianza kuugua tena safari hii alipatwa na ugonjwa Wa kansa ya shingo ya kizazi. Kwa bahati mbaya haikujulikana mapema kwakuwa walichelewa kwenda hospital kwa kukosa pesa muda huo. Walipo kuja kugundua kuwa anaugonjwa huo ulikuwa umeshaenea sehemu kubwa ambapo alilazimika kutoa kizazi. Hapakuwa na njia mbadala wote walikubaliana ili kuokoa maisha ya Mama lakini hadi wanafikia kutoa kizazi Zuu alikuwa Ana umri wa mwaka mmoja na miezi Tisa. Huzuni kwa mara nyingine ilichukua nafasi kwa wanandoa wale lakini walikubaliana na matokeo. Walimshukuru Mungu,Kuanzia hapo walielekeza macho yao kwa mtoto wao wapekee Zulpha.
Baba alikumbuka hayo wachache juu ya mtoto wao kisha aliunganisha na lile la Zuu kupenda kimapenzi John aliona anamtihani mkubwa sana katika kutatua swala lile. Hakuwaza juu ya chuki za mkewe kwa John ila aliumiza kichwa zaidi swala hilo.
Wakati inaendelea kuwaza Mara bosi wake aliingia ofisini kwake kuchukua kazi aliyomuachia.
"Nilikupa kazi ya dakika 15 ila nizaidi ya masaa ma nne sasa hujaniletea hadi niifate? Je! Huu niutandaji sahihi wakazi?" Alimhoji bosi wake ambaye alionyesha kukasirishwa sana na utendaji wake wa kazi kwa siku Ile.
"Samahani sana bosi kwa kuchelewesha lakini...mmmm....! Nao...na...na....naomba unipe dakika tano nitakurete."
"Nipe niondoke nayo..." Bosi alizidi kumbana koo
"Sijaimaliza bosi naomba dakika tano tu itakuwa tayari. "
"Nasema nipe kazi hatakama haijamalizika" Mr.Shaban alimpa bosi wake kazi isiyofanywa. Bosi alimtazama kwa jichokali baada ya kuipokea Ile kazi kisha alimwambia.
"Kwa uzembe wako umeisababishia kampuni upotevu wa milioni 350. Ni wazi kwamba umeshindwa kazi" aligeuka na kuondoka kwa hasira huku akiufungua mlango kwa ghadhabu sana.
Mawazo yalizidi kumuandama Mr.Shaban Mara baada ya bosi wake kuondoka hakukuwa na lenye unafuu kwa yale yaliyokuwa yakimuumiza kichwa. Swala la kazi lilikuwa linaumuhimu pia kuhusu familia kulikuwa na umuhimu zaidi. Kabra ya muda wakuondoka kazini kufika Mr.Shaban alisaini kisha aliondoka kurejea nyumbani. akiwa njiani aliwaza kuwa Hana kazi tena alitamani kumpigia Simu bosi wake ili amuombe msamaha ila moyo ulisita.
Alipofika nyumbani alikuta mazingira ya chumbani yamebadilika kabisa, kitandani kulikuwa na mkewe Mama Zuu amekaa pia pembeni yake kulikuwa na mabegi mawili makubwa yalioonyesha kusheheni nguo. Alivuta hatua chache kuelekea ndani kama ananyata huku akili yake ikihisi kama anaota, hatua zile zilimfanya ampite mkewe hadi upande wapili kisha aligeuka na kumtazama. Kabla haja zungumza chochote aligeuka tena,akafungua kabati languo alibahatika kuziona nguzo zake na chache ze mkewe ambazo zilikuwa zimechakaa. Bila kujitambua alijikuta anaingiza mkono kwenye mfuko wa suruali kisha kutoa kitambaa na kujifuta jasho lililokuwa likimtiririka, alipomaliza kujifuta alirushia kitandani. Mkewe ingawa alikwazika ila kwa kitendo kile alijikuta anacheka ghafla huku akitazama kitandani aliporusha kile kitambaa, mume hakujua kuwa mkewe anachekea nini alihisi ni dhara ila aligeuka na kutazama pale mkewe alipotazama ndipo aliposhituka kumbe hakikuwa kitambaa ila alitoa pesa noti za elfu kumi kadhaa na kujifutia ila hakulitambua kutokana na kuchanganyikiwa.
"Mabegi haya unamaanisha nini...!?" Aliuliza kwa sauti ya upole sana
"Ukiona Giza linazidi ujue kunakaribia kupambazuka"
"Unamaanisha nini...!?"
"Wewe ni mtu mzima sizani kama kunakigeni kwako hapa na kama kipo kigeni basi pole ila kwa ufupi naomba TARAKA yangu niondoke..."
"Ta...ta..tar.... Sijakuelewa au sijakusikia vizuri...!?" Aliuliza kwa mshangao
"Hayo masikio yanamatege? Kutosikia huko umeanza Leo? Umekuwa kiziwi au!? Nimekwambia nipe TARAKA yangu niondoke maisha yamenishinda" alizungumza kwa dharau Sana vile alivyokuwa akizungumza alikuwa anaongea kama na hawala yake na si mume wake.
"Mke wangu....! Yametoka wapi yote hayo......! Matatizo ya familia ndiyo yanakufanya ukimbie!? Hebu kumbuka mkewangu..., ulikula kiapo kuwa utaishi nami kwa kila Hali,kwa kila nyakati, pia tambua mke Bora ni Yule anayejitambua na kuwajibika katika Ndoa kama nafasi yake inavyohitaji awajibike. Sasa unajenga sura gani kwamimi mumeo ninapokuona unakimbia Ndoa kisa mtihani mdogo namna hii...!? Hukumbuki mazito tuliyopitia nyuma?" Maneno hayo yalitongolewa kwa busara sana toka kwenyekinywa cha Mr.Shaban hata hivyo Miriam (Mama zuu) wala hayakumuingia akilini.
" nawewe hayo yote yanatokea wapi? Nimekwambia nahitaji nini ila wewe unanieleza upuu.....!" Ghafla mama Zuu alikatisha mazungumzo baada ya kupokea Kofi toka kwa mmewe.ni makofi kadhaa aliyommiminia kisha alimwambia
" sasa unaruhusiwa kuondoka,nenda unakotaka kwenda." Alipokwisha kuongea hayo Mr.Shaban alitoka kwa hasira hadi nje na kujiegesha kwenye ukuta ulioinuliwa washani kwenye varanda ya nje. Akiwa hapo alimuona John kwa mbali kidogo amekaa kwa kujiinamia, alimfata kisha alizunguza naye
" John kinana wangu kunakipi kinachokusibu nje ya lile ulilotueleza?" Alimuuza kwa ustaarabu
"Baba, naumia sana. Naumia kwa mengi Baba yangu. Kwanza najitambua Mimi ni mtoto wakiume halafu umri wangu unaruhusu kujitegemea sasa kwanini naendelea kuwa chanzo cha ugomvi na upotevu Wa amani kwenye nyumba hii wakati njia ya kutatua hilo ipo!? Naumia kwakweli inafikia kipindi siwezi kuzungumza yote kwakuwa nitasababisha ugomvi kitu ambacho sipendi nyinyi ni wazazi wangu, Baba nipeni Uhuru kijana wenu nikajitegemee." Ni maneno makali yalitongolewa kwa uchungu sana. Baba alisikiliza aliona kazi kweli anayo.
" John Mimi ni Baba yako na Yule ni Mama yako. Lakini nakupa elimu hii ambayo itakusaidia sana maishani mwako. Siku zote mwanaume kunawakati huwa hamsikilizi mwanamke wala hashirikiani naye katika Jambo lolote. Mwanaume hufanya hivyo pale linapojitokeza tatizo zito ambalo linahitaji maamuzi magumu. Hapo wanawake kujiweka nyuma na kuelekeza macho kwa mwanaume kuona nini atafanya. Hapo hapo ukifanikiwa utakuta anakusifia ila ukishindwa lazima akulaumu au kukudharau, anasahau kabisa kama yeye alishindwa. Unanielewa vizuri lakini?"
"Nakuelewa Baba"
"Nimekutolea mfano huu ili utambuwe kuwa wanaume tumeumbiwa mazito. Mazitohayo siyo tu mizigo yenyekilo nyingi ila hata kutatua matatizo kwenye familia zetu na jamii zilizotuzunguka. Achana na wanawake wale, usilipokee kila litokalo kwao na kulifanyia kazi, jitahidi kuchambua mambo kisha toa maamuzi. Matatizo hayakimbiliki mwanangu. Leo hapa unajiona mtoto utakimbia kesho ukioa halafu likakutokea utalitatuaje? Au utalikimbia tena? Nimetoka kumuadhibu Mama yako kwasababu amesahau wajibu wake lakini wewe nakuadhibu kwa kukupa elimu hii ila ukishindwa kunielewa basi utaadhibiwa na ulimwengu. Nakusihi yapuuze hayo lakini Mimi naendelea kuyafanyia kazi pia nitashirikiana nawe pale unapohitajika ili mambo yaende sawa."
"Lakini Baba, Mimi nafanyiwa hivi kwasababu siyo mtoto wa....."
" shiiiiii.....!!!, usithubutu tena kuzungumza hicho ulichotaka kuzungumza halafu kifute akilini kabisa sawa?"
" sawa Baba nimekuelewa "
Nibaada ya mazungumzo ya muda kidogo ndipo John alipoonja tone la furaha kisha kujiona yupo nyumbani kama mwanzo. Alimpenda sana Baba yake kama Baba alivyokuwa akimpenda yeye. Alikuwa anamsikiliza na kumuunga mkono si tu kwakuwa ni Baba yake ila alikuwa anampenda kuliko Mama.
Jioni ile Mr.Shaban alimuita mwanaye kisha kuzungumza naye, kikubwa alichomwambia ni kwamba alimtaka atulie kwani kunamazito yanayoendelea kwenye familia. Hakupenda mwanaye aendelee na kitabia chake chakumsumbua John pia kutoshiriki baya lolote atakaloambiwa na mamaye.
'USIKU NI MREFU' kauli hii inamaana kubwa sana kwa wanandoa maana hutumia muda huo kujadili mengi yanayohusu mahusiano yao changamoto, matatizo na jinsi wanavyotakiwa waishi bila kusahau lile swala letu muhimu ambalo liliwafanya waitwe wanandoa. Ahahaaa mnataka nitaje? Waone...... mengine hayatajiki nisije nikawa bubu bure.
Jambo lakushangaza msemo huo ulikuwa kinyume (USIKU NI MFUPI) kwa wanandoa wale ndani ya siku Ile kwani Baba alijitahidi kuzungumza na Mama ili wayamalize na awaze kuhusu kazi lakini Mama hakumuelewa. Alijaribu kutumia njia yakuomba mchezo lakini hakufanikiwa, Giza lilizidi hatimaye Nuru ilishika anga.
Mihangaiko iliendelea huku nyumbani kukiwa hakuna amani. Baba alijitahidi sana kuiweka sawa familia yake ila upungufu wa ushirikiano wa mkewe ndio uliokuwa unamfelisha.
Siku ya Tatu Mama alikubari yaishe na kuungana na mumewe kuendelea kujenga familia yao. Ilikuwa ni saa nane ya usiku ambapo ghafla Mr.Shaban alikuwa na furaha baada ya mkewe kuonyesha amesamehe yote. Usiku huo huo refa alipuliza kipenga mechi ilichezwa kwa ushindani mkubwa na ilikuwa yakipekee kwani kila mmoja alikuwa anamkamia mwenzie kwa muda mrefu. (Mmmm tusiingie ndani sana huko.)
Asubuhi na mapema Baba aliamshwa ajiandae kama ilivyo mwanzo ili awahi kazini kweli Mr.Shaban alikuwa na furaha iliyompelekea kuwa na hamu ya kazi. Alijiandaa mapema akanywa chai kisha alielekea kazini. Akiwa wakwanza kufika ofisini ilimbidi asubiri mwenye funguo afike kwani aliwahi sana. Wafanyakazi wengine walipofika walishangaa kumuona Shaban amewahi sana na alikuwa anafuraha tofauti na siku chache Ilizopita.
Mr.Shaban alipigwa na butwaa baada ya kuiona bahasha ndogo mezani kwake alipoifungua kulikuwa na barua imetoka kwa bosi wake ambapo ilikuwa yakumsimamisha kazi kwa muda usiojulikana.
USIKOSE SEHEMU YA 003
Kwa ushauri ushauri na maoni no. 0716883222
Plz comment , like, and share ndio mshahara wangu toka kwako msomaji wangu mpendwa. Nawapendeni na kuwajali wote. Siku njema. Ahsante.
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO EmoticonEmoticon