MAANDALIZI BORA YA KUPATA MTOTO KWA WANANDOA

10/05/2016 10:32:00 am
 MAANDALIZI BORA YA KUPATA MTOTO KWA WANANDOA
Na: Fraidy Mtemah.



maandalizi bora siku zote huleta kitu bora. harikadharika katika swala la kutafuta mtoto kwenye ndoa.


nianze na mazingira mabaya ambayo wanandoa hutumia kumtafuta mtoto. ni kwamba:-

baadhi ya wanandoa hawana mawasiliano mazuri katika tendo la ndoa. utakuta marumbano yao ya kupishana kauli kutokana na changamoto mbali mbali za maisha wanazipeleka hadi kitandani.

utakuta wanagombana mchana kisha kila mmoja anategeshea usiku amkomeshe mwenzie. kwakuwa asilimia nyingi wanawake wanazidiwa nguvu anaweka kisirani kwa kusema leo akiomba tendo simpi, wakati huo huo mwanaume anawaza usiku lazima ampe tendo, endapo asipompa atachukulia kama kigeazo na kuendeleza ugomvi.

mazingira kama hayo utakuta tendo linafanyika huku kila mmoja akiwa hajaridhika ila anatimiza wajibu tu. kwa bahati nzuri au mbaya ni siku ambayo mwanamke anashika ujauzito. AU Ndoa imekuwa ya ugomvi kila kukicha hata katika kumtafuta mtoto wanafanya tendo ilimradi tu atimize wajibu.

katika hali ya kawaida mazingira kama hayo wala siyo rafiki kwa ujauzito pia hata mtoto ajaye.

kuna mambo machache ya kuzingatia kwenye ndoa wakati mnatafuta mtoto ili kumpata mtoto atakayekuwa chachu ya furaha ndani ya nyumba siku zote.

kabla hamjaanza kumtafuta mtoto anzeni kutengeneza mazingira rafiki ya kumpokea mtoto. hakikisheni nyote mnakuwa na furaha,ikiwezekana itengenezeni furaha hiyo kwa wiki nzima au mwezi mzima. muishi kama vile penzi lenu lilivyoanza kuchanua hadi kila mmoja ashangae na kuona kunautofauti flani. furaha ikishatawala ndani ya nyumba,shirikianeni kujadili swala hilo na kila mmoja aeleze vile alivyokuwa tayari kupokea hali hiyo. wote mkishakubaliana na kuona kila mmoja ameliafiki sambamba na kuwa na hamasa nalo,zungumzeni kuwa mnataka mtoto wa jinsia gani.


 wakati mnazungumza kuhusu jinsia ya mtoto, mke anatakiwa azifahamu kwa kina tarehe za mzunguko wake. ingawa binadamu siyo mpangaji juu ya upatikanaji wa jinsia ya mtoto ila ni wazi kuwa ukienda vizuri na tarehe basi unaweza kupata jinsia husika. ikitokea mke ameshika ujauzito msijijengee akilini (uhakika) kuwa atazaliwa mtoto wa jinsia flani maana ikiwa tofauti utakuwa na chuki dhidi ya mtoto aliyezaliwa.

Mshirikisheni Mungu kabla ya tendo na baada ya tendo. Wanandoa hawana tabia ya kumuomba Mungu ili tendo Lao liwe salama na lenye heri. Wapo pia wanaomsahau Mungu hata wapatwapo na matatizo hali inayowapelekea wachukue maamuzi mabaya pindi dosari inapoingia kwenye Ndoa. Yatupasa tutambue Mungu ni kila kitu hivyo hata katika kumtafuta mtoto yatupasa tumtangulize.

Akishashika ujauzito, Tengeni muda wa kuriwadhana. Mama mjamzito anahitaji faraja muda wote. Hapendi buguza hivyo Baba unatakiwa utenge muda Wa kukaa na mkeo,usijifanye upo bize na kazi au unamaliza muda wako kwenye michepuko siyo vizuri. Yawezekana kweli ukawa na michepuko ila mpe nafasi mkeo na usimdhihirishie kama unamchepuko au kumtengenezea mazingira ya yakukushuku.

Baba jitahidi kuwa na maneno matamu kila Mara kwani kunawakati mama mjamzito hujikuta anakuwa na lugha chafu au kukuchukia mumewe, lakini usichukulie kama sababu,cheza kwenye part yako kama Baba kwa kutekeleza wajibu wako kwake. Furaha anayoipata Mama humshirikisha na kiumbe kilichopo tumboni. Ambapo atazaliwa mtoto mwenye asili ya furaha.

TENGENEZENI MAZINGIRA RAFIKI YA KUSHIKA UJAUZITO, MAZINGIRA RAFIKI YA KULEA UJAUZITO, MAZINGIRA RAFIKI YA KUPOKEA MTOTO KWA KUMSHIRIKISHA MUNGU. hakika atakuwa ni mwenye furaha muda wote. Amina

By #Fraidy

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO EmoticonEmoticon